-->

Sizai Hadi Ndoa Kwanza- Dr. Sandra wa Siri Za Familia

MWAJABU Omary ‘Dr. Sandra’ mwigizaji anayetamba katika tamthilia ya Siri za familia amefunguka kwa kusema kuwa pamoja na kuwa na mchumba wake zaidi ya miaka mitano katika mahusiano lakini hawezi kumzalia watoto hadi akimuoa na kufunga ndoa.

Dr. Sandra katika pozi

“Najua mchumba wangu ananipenda sana na nipo nnaye zaidi ya miaka mitano, lakini sitaki kuzaa nje ya ndoa kwani sisi wasanii mara nyingi ndio kioo cha jamii hivyo hutakiwi kukosea hesabu,”

Muigizaji huyo amedai kuwa anatamani kuzaa watoto watatu na kati ya hao wanaume wawili na wa kike mmoja ndio anatakuwa ametimiza ahadi yake, msanii huyo anaamini kuwa umaarufu alio nao kupitia tamthilia hiyo ni kuendelea kuongeza mashabiki kwa kuwa na tabia ya mfano mzuri.

Msanii huyo anasema kuwepo katika kundi la Siri za Familia amejipatia faida nyingi sana ikiwa ni pamoja na kufanikisha biashara zake ambazo wateja wamekuwa wengi kutokana nay eye kuonekana katika tamthilia hiyo ambayo urushwa kupitia Runinga ya East Africa Tv.

Filamucentral

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364