Wanafunzi Wenzake Norah Waamsha Vilio Msibani
Dar es Salaam. Vilio na simanzi vimetawala kwenye msiba wa mtoto Norah Marealle baada ya kuwasili kwa wanafunzi wenzake wa Shule ya Atlas ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi hao waliwasili saa tano nyumbani kwa kina Norah eneo la Sinza Mori.
Nora ambaye amefariki dunia jumapili iliyopita huku kukiwa na madai kwamba alibakwa na kisha kunyongwa kabla la kufa, anazikwa leo baadaye katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Picha na GPL