-->

Snura aweka wazi mahusiano yake mapya

Msanii wa bongo fleva, Snura Mushi maarufu kama Malkia wa uswazi amefunguka kwa mara nyingine na kudai yeye hana roho ya ubinafsi kama walivyo watu wengine kwenye kutoa msaada kwa watu ambao wanahitaji kufikia malengo yao waliyojiwekea.

Snura ametoa msimamo wake huo katika ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya watu kuendelea kutoa maneno yao kuhusiana na picha iliyosambaa mitandaoni ikimuonesha ana-kiss na mvulana aliyetambulika kwa jina la Minu Calypto licha ya hivi karibuni  kulizungumzia sakata hilo kwenye kituo cha EATV ambapo mpaka sasa kuna baadhi hawaja amini kile alichokielezea.

“Kuna muda tunasema ndio kuna muda tunasema sio inawachanganya mpaka mnabishana hadi kwa watu wetu wa karibu kuamini kisicho sahihi ila penye ukweli, uongo hujitenga”, amesema Snura.

Pamoja na hayo, Snura ameendelea kwa kusema “majibu yote ya picha ya ‘kiss’ mlizoona na kila kitu yanakuja, wakati mwingine mlichokifanya kwenye kazi kinatoka nje kabla na kupelekea kuchanganya watu. Ila hapa hakuna mapenzi kuna kazi tu, hamjui kwa nini nimejitoa kumsaidia na kumsaidia mtu sio mpaka awe bwana ako, ubinafsi huo mimi sina na kwa kuwa nimejitolea kumsaidia basi nakubaliana na kuvumilia yote”.

Kwa upande mwingine, Snura Mushi amewasisitizia wanaoendelea kuijadili picha yao hiyo kuwa hatoweza kubadilika Minu Calypto kwa kuwa huyo ni mdogo wake.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364