-->

Ray, JB Waapa Kutoana Meno Pasaka!

WAKALI wa filamu za kibongo nchini, Vicent Kigosi ‘Ray’ na Jacob Stephen ‘JB’ wameapa kupasuana vilivilivyo katika pambano la raundi nane ambalo siyo la ubingwa lilipangwa kufanyika usiku wa pasaka kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Mbali ya manguli hao wa filamu nchini kutoka katika kiwanda cha Bongo Muvi, Bondia Twaha Hassan wa Morogoro  ‘Kiduku’ anatarajia kuzichapa dhidi ya Chimeme Chiota  kutoka Malawi katika pambano ambalo litakuwa na raundi kumi huku likitarajia kuw na upinzani mkali  kutokana na upinzani wa  rekodi za mabondia wote wawili.

Katika  mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar ambapo JB alisema kuwa lazima atamchakaza vikali mpinzani wake Ray kwa kuwa amemzidi kwa kila kitu huku Ray akisema atahakikisha amapasua vilivyo kutokana na maandalizi atakayokuwa ameyafanya.

Kwa  upande wa promota wa pambano hayo ya aina yake, Siraji Kaike alisema kuwa ameamua kuwakutanisha wasanii hao  ulingoni kutokana na mara nyingi kutambiana hivyo anaamini watatoa upinzani mkali ambao utamaliza ubishi wao wa muda  mrefu ikizingatiwa ni mashabiki hasimu wa Simba na Yanga.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364