-->

Snura Kuwafurahisha Mashabiki Mwakani

MSANII Snura Mushi ‘Snura Majanga’, aliyewahi kuwika na nyimbo mbalimbali, ameibuka na kudai kwamba ana mpango wa kutoa filamu moja mwakani.

snura-1

Snura Mushi ‘Snura Majanga’

Snura alisema baada ya kuingia katika muziki amekuwa na shoo nyingi kiasi kwamba hukosa muda wa kuigiza, licha ya mashabiki wake kumtaka afanye hivyo hata kwa mara moja.

“Mashabiki wangu wamekuwa wakinitaka angalau nicheze hata filamu nmoja, lakini shoo za muziki zimekuwa nyingi nakosa muda wa kuigiza, lakini nitapanga mwakani nitoe filamu moja kwa ajili ya mashabiki wangu huku nikiendelea na muziki,’’ alisema Snura, ambaye amekuwa akiingiza fedha nyingi kupitia shoo zake za mara kwa mara mikoa mbalimbali.

Snura ameigiza filamu mbalimbali na mwanzo wa safari yake ya sanaa aliwahi kuwa kundi moja na marehemu Sharo Milionea na Kitale.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364