-->

Uzee Kumwachisha Bi Mwenda Uigizaji

MUIGIZAJI mkongwe kwenye Tasnia ya Filamu Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ amefunguka kuwa anaona uzee umeshamfikia hivyo muda si mrefu ataamua kupumzika kuigiza ili afanye kitu kingine kulingana na umri wake.

bimwenda

Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’

 

Akizungumza na gazeti hili, Bi Mwenda alisema amecheza filamu muda mrefu takriban miaka ishirini hivyo anaona wazi atashindwa kukimbizana kwenye kambi kwenda huku na huko kutokana na umri wake hivyo anajipanga kuangalia afanye nini.

“Kweli kabisa nikijiangalia uzee umeshagonga hodi na siwezi kuukimbia ila kwa sasa najipanga nipumzike kwani ni muda mrefu niko kwenye sanaa, nitaangalia nifanye nini ili kipato changu kiendelee,” alisema Bi Mwenda pasipo kuainisha atasimama baada ya muda gani.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364