-->

Snura Mushi: Natamani Kufumaniwa

KATIKA hali ya kushangaza mkali wa wimbo wa ‘Chura’ wenye mahadhi ya Singeli, Snura Mushi ‘Snura Majanga’, amedai kwamba anatamani afumaniwe.

snura421

“Sijawahi kufumaniwa ila natamani nifumaniwe ili nijue uchungu na changamoto zake maana ili uweze kusimulia kitu vizuri sharti kikutokee,” alieleza Snura.

Pia Snura alifafanua kwamba licha ya kutokuwahi kuolewa ana watoto wawili huku akiongeza kwamba ndoto yake ni kuwa na mume mwenye imani.

“Sipendi wanaume wa kunioa wawe kama Chura niliyemuimba, napenda nije kupata mwanaume wa kunioa anayemjua Mungu, atakayekuwa na hofu ya Mungu,” alieleza Snura.

Katika hatua nyingine, Snura alisema anapenda kuutumia muda mwingi kutembelea watoto yatima na kutoa misaada midogomidogo kwa familia za chini kwa kuwapa sukari, sabuni, vyakula na nguo.

“Kwa sasa nina madrasa kwa ajili ya kutoa mafunzo ya dini kwa watoto 150, nagharamia malipo ya walimu na pia vitabu vya watoto hao,” alieleza Snura.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364