Nilimpeleka Mama Ulaya Kumtoa Ushamba – Diamond
Msanii wa Bongo flava Diamond Platnumz alitembelea nchi karibuni tisa za ulaya katika ziara yake ya kimuziki aliyoimaliza hivi karibuni.
Amesema ameona kuwa mziki wa bongo flava umekuwa mkubwa sana duniani kwani alijaza kumbi ambazo hata baadhi ya wanamuziki wa Marekani wakifika wanafanyia kule kwa sababu sio kila msanii wa marekani anaweza kujaza Arena hizo.
Msanii huyo amesema hii ni mara yake ya kwanza kusafiri na familia yake, kama mama yake hajawahi kwenda ulaya kabisa hivyo ameamua kumtoa ushamba.
“Miaka inaenda na tangia ‘nimetoboa’ sikuwahi kusafiri na mama yangu kwanza hakuwahi kwenda Europe au Ulaya alikuwa anaisikia tu kwenye bomba, inaweza kuwa kesho au kesho kutwa nikadondoka nikafa halafu mama yangu akabaki tena kuisikia nikaona ni bora kwenda kutoana ushamba kabisa”
Aidha msanii huyo amesema ataendelea na ‘tour’ yake ambapo atafanya ‘show’ 3 marekani, na pia ‘show’ nyingine zitafanyika India, Dar es Salaam , Mwanza, na Australia.
Diamond ameongeza kuwa atakuwa na ‘tour’ rasmi kwa ajili ya Afrika na amesisitiza kuwa kuna nyimbo anasubiri zitoke maalum kwa ajili ya Afrika.
Eatv.tv