Snura: Tuache Kugombea Mabwana Tufanye Kazi
SNURA Mushi mwigizaji wa filamu na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya amewaambia waigizaji wa kike wasiwe tegemezi kwa kufanya kazi zinazoandaliwa na watayarishaji wa kiume wakati nao wanaweza kuetengeneza filamu.
Msanii huyo anatiririka kwa kusema kuwa badala ya kutumia muda mwingi kugombea mabwana wajipange kufanya kazi na kwa kiwango kikubwa kwani wanakubalika katika soko lakini hawalitumii sasa iwe basi kusubiri wasaidiwe.
“Jamani tuamke na kufanya kazi zetu kama watayarishaji wa kike maana wanaume wanatuona kama hatujielewi na tunawategemea wao waandae kazi tucheze sisi hatuwezi kuwachezesha wao?,”anauliza Snura.
Snura anasema kuwa anaamini iwapo wataungana na kuandaa filamu ya kuwashirikisha nyota wote wa kike lazima kazi hiyo itauzwa sana sokoni na kutoa njia kwao kama waigizaji wa kike kusimama kama watayarishaji tofauti na ilivyo sasa waandaaji wengi ni wa kike.
FC