Steve Nyerere Afungukaia Urais wa Mwakifamba Shirikisho la Filamu Tanzania
Mchekeshaji Steve Nyerere amendelea kuwachana wasanii wenzake kutotumia nguvu nyingi kutaka kumng’oa madarakani Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba kwa kisingizio cha kudai harakati za kufanya mabadiliko katika tasnia ya filamu.
Steve ametema chehe hizo kwa kudai figisu zinazofanywa na wasanii wenzake kwa njia za maadamano zina lengo la kutaka kumuondoa madarakani Simon Mwakifamba ila kwakutumia kigezo cha kupambana na wamachinga kitu ambacho hakileti maana katika jamii.
“Simon Mwakifamba siyo Rais wa Dar es salaam tu bali Tanzania nzima, sasa watu wa Dar es salaam, wasanii wa Dar es Salaam mnapojichukulia hatua za kufanya maandamano pasipo kuwashirikisha watu wa mikoani lazima mtaonekana watu wa Dar es Saalam ni upepo tu uliowasukuma, fashion au kujitafutia umaarufu kitu ambacho hakileti sifa nzuri” alisema Steve.
Aidha Steve aliendelea kusisitiza kwamba “Mnatumia nguvu kubwa sana kumtoa mtu kwenye cheo chake kwa kile mnachokiita harakati kwani mliambiwa yeye hataki hizo harakati? Cha msingi niwashauri wenzangu tukaeni kikao kikubwa na wenzetu wa mikoani tumuite Rais wetu tumwambie matatizo yetu naye atatusaidia kutatua kilio chetu”– Steve aliendea kusisitiza.
Katika hatua nyingine Steve ameongeza kuwa kuwepo kwa changamoto za wasambazaji nchini ndio chanzo cha kiio cha wasanii wengi hali inayowafanya wasanii kugombana na machinga.
“Sisi waigizaji tunauza ‘master’ kwa wasambazaji sasa kwa nini mimi nilipishwe kodi na makato yasiyoeleweka. Wasambazaji ndio wanaotakiwa kubanwa na kwa vile wasambazaji wapo wachache ndio maana tunanyonywa ingekuwa wapo wengi tungekuwa tunaringa sana. Hebu tusigombane na wamachinga tumbane msambazaji atuambie shida ziko wapi katika filamu zetu”- Steve alimaliza.