-->

VIDEO: Rais Magufuli Afuta Ajira Zaidi ya Elfu Tisa

Rais  Dk. John Pombe Magufuli, ameiagiza Wizara ya Fedha kufuta mara moja ajira za  watumishi wa umma 9,932 waliobainika kughushi vyeti, kwenye orodha ya malipo ya watumishi wa umma.

Akiongea leo mara baada ya kupokea ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma mjini Dodoma, Rais Magufuli pia amewataka watumishi hao kuondoka wenyewe na iwapo watakaidi wakamatwe na vyombo vya dola na kushtakiwa.

Rais Dk. Magufuli pia ameziagiza mamlaka husika kujumuisha nafasi 9,932 za ajira ambazo zimeachwa wazi na watumishi wa umma walioghushi vyeti, kwenye ajira mpya zaidi ya elfu 52 za serikali ili ziweze kuchukuliwa na watu wenye sifa na uwezo wa kumudu nyadhifa zilizoachwa.

Akizungumza wakati akiwasilisha ripoti hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, amesema, kwa Mujibu  wa Kanuni na Sheria za nchi zinabainisha wazi kuwa mtu atakaebainika kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo adhabu yake ni pamoja na kifungo cha Jela.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364