Steve Nyerere Awapongeza Harmonize na Iyobo kwa Hili
Kiongozi wa zamani wa Bongo Movie Unit, Steve Nyerere amempongeza msanii wa muziki, Harmonize pamoja na dancer wa Diamond, Mosei Iyobo kwa kuwapa utulivu wasanii wenzake wa filamu Aunt Ezekiel na Jacqueline wolper.
Muigizaji huyo ambaye alikuwa MC katika iftar ya GSM iliyofanyika Kigamboni weekend hii na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali, alisema anawashukuru wasanii hao wa muziki kwa uwamuzi wa kuwahifadhi dada zake hao.
“Mimi nashukuru wasanii wa bongofleva kwa kuwahifadhi dada zetu, Aunt yupo poa, na Wolper naona safi,” alisema Steve Nyerere huku akicheka.
Wolper na Harmonize kwa sasa ni wapenzi na kila mmoja anaonyesha anampenda mwenzake, na Aunt Ezekiel na Mose Iyobo ni wapenzi wa muda mrefu na wanaishi kama familia na mtoto wao mmoja aitwae Cookie.
Bongo5
NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA