Rammy Apata ‘Shavu’ Hili Ghana
Staa wa Bongo Movie, Rammy Galis ‘Pacha wa Kanumba’ amezidi kula mashavu katika Tasnia ya Filamu Ghana na hivi karibuni anatarajiwa kudandia pipa kuelekea nchini humo kwa ajili ya kugonga filamu nyingine na dairekta maarufu nchini humo anayejulikana Afrika nzima.
Akichonga na gazeti hili Rammy Galis alisema filamu alizofanya na wasanii kutoka Ghana na Nigeria ambazo ni Red Frag, Her Shoes na Cris Cross ndizo zimemfanya kupata jina zaidi Afrika Magharibi hata kuendelea kupata mashavu hayo lakini pia yuko katika maongezi mazuri na prodyuza Sylivester Madu ‘Rambo wa Nollwood’ aliyekwishafanya naye kazi awali ili wapige mzigo tena.
“Kwa sasa filamu ninayokwenda kucheza Ghana ni sapraizi lakini wapenzi wa kazi zangu watarajie kitu kikubwa sana na wasanii maarufu kutoka huko na kazi ikiwa tayari nitawaeleza. Kikubwa ninaomba wapenzi wa filamu wanisapoti maana kwa sasa mimi ndiye Mtanzania pekee ninaye komaa kwenda nje,” alisema Rammy Galis.
Chanzo:GPL
NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:
Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.
Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA