-->

Sura yangu Haijakomaa, Bado Mrembo-Shamsa Ford

MUIGIZAJI wa filamu Bongo movie Shamsa Ford katoa mpya pale aliposema kuwa bado yu ngali kijana kwani akijiangalia uso wake bado na sura yake ina mvuto na kumuweka katika makundi ya wadada wadogo kabisa, anafurahia kwa muonekano huo ambao anahisi hakimbizani na uzee akijiangalia uso wake.

“Mpaka rahaa jamani nilikuwa najiangalia katika kioo kumbe uso bado haujakomaa name bado nipo katika kundi la warembo ukiwa na sura isiyokamaa hadi unajidai maana ukikomaa sura inakupoteza,”alisema shamsa.

Shamsa anasema kwa kucheka akiwa yupo katika hali ya utani kwani anaami mwanamke anapokuwa na mwili mnene ni rahisi sana kupoteza nuru na kuonekana tofauti na urembo ambao unatoweka hasa pale uso eti ukikomaa na kuonyesha sura ya kiutu uzima zaidi.

Filamucentral

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364