-->

Tamko la Wasanii Wakongwe Kwa Rais Wa Shirikisho La Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba

 

WASANII Wakongwe katika tasnia ya filamu Swahilihood leo tarehe 16Th December, 2015 katika ukumbi wa Idara ya Habari ya Maelezo wametoa tamko lao kuhusu kumtaka Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba kugombea nafasi hiyo ambayo alitangaza kutoshiriki kugombea nafasi hiyo kwa kipindi kijacho uchaguzi huo mwezi huu 2015.

Wasanii wakongwe wakitoa tamko lao kuhusu Rais Mwakifwamba

Wasanii wakongwe wakitoa tamko lao kuhusu Rais Mwakifwamba

Baada ya salamu hizo kwenu tumekuja hapa kwa tukiwa na ya kuwaeleza wanahabari sote mnatujua kwa kutuona au kuona kazi zetu kupitia katika filamu hata vyombo vyenu, kwanza tunaanza kwa kumpongeza Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais na utendaji wake sote tumeona na kutupa faraja kubwa sana kama Watanzania.

Pili pongezi zetu ziende kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Moses Nnauye kwa kuchaguliwa kuwa Waziri wetu na moja kwa moja tunaona Nuru kwetu ikija baada ya kuwa katika kipindi chenye changamoto nyingi tukiwa kama wasanii wakongwe hapa nchini Tanzania.

Baada ya utangulizi huu mzito wenye tija sasa tuseme kilichotufanya tuone haja ya kuongea na nyinyi wanahabari wadau wetu ambao tunaamini kabisa sauti yenu inafika mbali zaidi baada kuidaka na kuirusha katika vyombo vyenu yaani magazeti, redio, Runinga na mitandao ya kijamii kwa ujumla wake, sote tu mashahidi kuwepo kwa chombo chetu wasanii ambalo ni shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).

Shirikisho hili lina uongozi wake mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi kwa masikitiko makubwa Rais wa Shirikisho hili na mtendaji mahiri Bwana Simon Mwakifwamba alitangaza kutogombea tena nafasi ya Urais lakini sisi kama ndio Wasanii wakongwe katika tasnia hii tunapinga uamuzi wake na kumuomba abadilishe fikra hizo na agombee tena kwani tumeona Nuru imekaribia kwetu, baada kwa muda mrefu kukosa kitu kinachotuweka pamoja.

Waswahili usema mji usio na Wazee na kusikilizwa mji huo ukosa hekima na Busara na hatimaye uzaa madhara na kuleta uharibifu, kwetu tunaona hilo hatutoliruhusu litokee kwani mmekuwa mashahidi pale baadhi ya wasanii wakiongea vitu vya hovyo kabisa tena kwa migongo yetu bila kutushirikisha tunahitaji kiongozi mwenye upendo na kutuunganisha si wa kutugawaga, naye ni Simon Mwakifwamba.

Tumeshuhudia miradi mingi ambayo imehasisiwa chini yake na haijakamilika vema aingie tena kumalizia kazi aliyoianza, kuna TAFF TRUST FUND, pia TAFF CREATIVE LTD miradi hiyo yote inahitaji umakini mkubwa katika kuhakikisha inasimama na kutuokoa wasanii bila kusahau Sera ya filamu ambayo inasubiri kupitishwa na Serikali inahitaji mtu makini na mfuatiliaji kama Mwakifwamba.

TAFF TRUST FUND ni mfuko wa wasanii wa filamu ambao utatusaidia sana katika utendaji wetu ni kitu muhimu sana hakuna mtu aliyefikiria kuhusu wasanii wa filamu kuwa na mfuko wao, TAFF CREATIVE LTD huyu ni mkombozi kwetu kwani kazi zetu zimekuwa na changamoto kukosa soko la uhakika kampuni hiyo itasaidia kubororesha maslahi katika tasnia ya filamu Tanzania.

Tuna mengi lakini kwa leo nafikiri hayo yanatosha kwa kifupi pia nimeongozana na wenzangu wana yao ya kuongea tukimuomba Mwakifwamba abadilishe mawazo yake na kuendelea nasi tukiwa kama wazee wake washauri tunahitaji mtu ambaye atakwenda na kasi ya Rais wetu Dkt. Magufuli . Asanteni kwa kunisikiliza

Mratibu

WASANII WAKONGWE KATIKA TASNIA YA FILAMU

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Hi there!

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364