-->

TANAPA Kutoa ‘Location’ kwa Wasanii

MENEJA Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete, amesema wasanii wa filamu nchini wanatakiwa kutumia mandhari za asili zilizoko katika hifadhi za Taifa kwa ajili ya kurekodi filamu zao ili kutangaza utalii wa ndani.

TANAPA-Shelutete

Shelutete alisema hayo katika tamasha la chama cha wasanii wa filamu wa jijini Arusha (TFDAA) katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, akidai kwamba Tanapa itatoa ushirikiano kwa wasanii watakaoonyesha nia ya kurekodi filamu zao katika maeneo ya hifadhi ambayo ni salama na yenye mvuto mkubwa.

“Nchi yetu imejaliwa vivutio vingi hivyo wasanii washirikiane na Tanapa kuutambulisha utalii wetu ili ziweze kuchangia pato la Taifa,” alisema Shelutete.

Naye Rais wa Shirikisho la Silamu nchini (TAFF), Simon Mwakifamba, aliwataka wasanii watumie fursa ya maonyesho ya kimataifa ya filamu yanayojulikana kama Tanzanite International Film Festival yatakayojumuisha wasanii wa filamu kutoka nchi mbalimbali duniani kujitangaza na kutengeneza marafiki wakusaidiana katika sanaa zao.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364