-->

Subirini Ngoma ya East Coast Team – Mwana FA

Msanii mwana FA ameelezea sababu za kuvunjika kwa kundi la East Coast Team na kutoa taarifa za kurudi kwake, na kuwataka mashabiki wakae tayari kwa muda wowote kupata kazi kutoka kwao.

MWANAFA-NEW

Mwana FA ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, na kusema kuwa majukumu ndiyo yalifanya kundi hilo kusambaratika kikazi, lakini kwa sasa East Coast Team imesharekodi wimbo, kilichobaki ni kwa wao kuiachia watu waipate.

“Unajua East Coast kina AY na GK ndio walianzisha mi niliingia baadae na kina Oten, wakati huo nishatoa ingekuwa vipi, majukumu mengi yanakuja, sasa ikawa O Ten akifanya vitu mnaanza kuulizwa mwenzenu kafanya hivi, unabeba compliment na mizigo ya watu wengi, na kwa sasa hivi hela ambayo mi nalipwa na AY anayolipwa, GK na kisha team nzima, lazima watu wafanye kazi independent ili kuleta mkate, lakini nisikudanganye tumesharekodi ni time tu ya kuitoa tu”, alisema Mwana FA.

Pia Mwana FA amemuongelea mmoja wa wanaounda kundi hilo la East Coast Team, ambaye amekuwa kimya sana kwenye game, na kusema O ten yupo na ndiye mtu mzuri ambaye anafurahisha anapokuwepo.

“OTen kama Ommy Crazzy chizi ambaye anaweza kutoka akili, yupo hyped kweli, lakini ni mtu mzuri kuna siku tumeenda Moro tukakutana lakini sijamuona tena”, alisema Mwana FA.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364