Tanzia: Bongo Movie Wampoteza Mwingine
TASNIA ya filamu hapa Tanzania, Bongo Movie wamempoteza muigizaji mwenzao Kijakazi Pazi Shabani maarufu kwa jina la Zamzam aliyefariki dunia jana Jumapili, Januari 1, 2017 mkoani Kigoma.
Chanzo cha habari hii kimeeleza kuwa mwili wa Zamzam unatarajiwa kusafirishwa leo kutoka Kigoma kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi ambapo msiba huo utakuwa maeneo ya Sokota, Temeke karibu na sheli.
Kifo cha Zamzam kimekuja ikiwa ni siku chache baada ya mwigizaji Gift John ‘Hidaya’ kuaga dunia mnamo Desemba 29, 2016 katika Hospitali ya Sinza ‘Palestina’ na mwili wake kuagwa kwenye Kanisa la Anglikana lililopo Njiapanda ya Segerea, Dar juzi Jumamosi.
Zamzam alikuwa mwigizaji wa Kundi la Kidedea ambapo alijinyakulia umaarufu mkubwa baada ya kucheza tamthilia ya Mchezo wa Kidedea, ambamo ndani yake aliigiza na marehemu Tabia huku baba yao alikiwa mzee Jengua.
Chanzo:GPL