Inasikitisha Sana, Tazama Nando wa Big Brother Alivyoathiriwa na Matumizi ya Madawa ya Kulevya
HALI ya kiafya ya mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Big Brother Afrika, 2013 nchini Afrika Kusini, Ammy Nando inasikitisha ambapo inadaiwa kuwa amedhoofika sana kwa sababu ya matumizi ya madawa ya kulevya.
Picha zinazoendelea kusambaa mitandaoni (picha ya juu kulia), zinamuonesha kijana huyo akiwa amedhoofika sana mwili wake, tofauti kabisa na jinsi afya yake ilivyokuwa hapo awali.
Kundi kubwa la vijana hasa mastaa hapa Bongo wanazidi kuangamia na wengine kufifisha ndoto zao za kimaisha kutokana na athari wanazozipata kwa kutumia ya madawa ya kulevya huku vijana wengi wakiharibikiwa maisha yao kila kukicha, na taifa likipoteza nguvu kazi yake.
Imeelezwa kuwa, kwa sasa hali ya afya ya Nando ni zaidi ya Chid Benz.
Chanzo:GPL