Tattoo Yangu ya Mgongoni Inasema- Amanda
STAA wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amesema tattoo yake aliyojichora mgongoni yenye maneno ‘Mapenzi yanauma’ ni kama inasema kwani mwanaume yeyote atakayekuwa naye kimapenzi, akiiona itampa kitu cha kujifunza.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Amanda alisema alijichora tattoo hiyo baada ya kuumizwa kwa muda mrefu na wanaume, hivyo anaamini atakayefuata hivi sasa, atakuwa makini kuhakikisha hamuumizi tena.
“Tangu nianze kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi niliwahi kupata mwanaume mmoja tu ambaye alilijali penzi langu, bahati mbaya alifariki dunia, baada ya hapo nimekuwa mtu wa kuumizwa tu,” alisema.
Chanzo: GPL