TCRA: Simu Feki Kuzimwa Leo
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA imesisitiza kuwa zoezi la uzimwaji simu feki unatekelezwa leo kama ilivyokuwa imepangwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye makao makuu ya mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu, James Kilaba alisema kwa wale watakaofanya ujanja wa kubadilisha namba tambulishi (IMEA) watachezea kifungo cha miaka 10 jela au faini ya shilingi milioni 30 au vyote.
“Simu bandia zimepungua hadi chini ya asilimia 5! Hakuna kuongeza muda. Simu bandia ukomo wake pale pale 16 Juni,” TCRA wametilia mkazo kwenye Twitter.