Tetemeko la ardhi lazua hofu kwa wananchi wa Bukoba
Hofu hiyo inatokana na tetemeko la ukubwa wa 5.7 kwa vipimo vya Richter lililotokea mkoani hapa Septemba mwaka jana na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 10 majeruhi takriban 200 na mamia wengine kukosa makazi.
Wananchi waliozungumza na gazeti hili, katika Manispaa ya Bukoba, wilaya za Missenyi, Muleba na Karagwe wamesema tetemeko hilo lilitokea saa saba usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wananchi mjini Bukoba walilazimika kulala nje ya makazi yao kutokana na kishindo cha tetemeko hilo.
Mwananchi