Tumenusurika kumwagwa damu – Shilawadu
Kupitia mtayarishaji wa kipindi cha Shilawadu kinachoruka Clouds Tv, Benedict Noel amebaisha kuwa kazi ya kukusanya material ya kipindi hicho ni kigumu kutokana na mambo wanayopitia wakati wa kutafuta habari ya kipindi husika.
Mtayarishaji huyo amebaibsha hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram wa kipindi hicho kwa kuandika mambo wanayokutana nayo na waliyokutana nayo hivi karibuni.
Kazi Yetu Ina Changamoto Kubwa Sana…. Asilimia kubwa Ya Ma Star wanatuunga Mkono, kwa kufanya maamuzi wanayoyataka kulingana na moods wanazokuwa Nazo tunapowafata bila kutudhuru
Ucku Wa Leo Wakati Tukiwa Kazini Tumenusurika Kumwagwa Damu na Mtu tuliemfata Kumuomba kufanya nae Mahojiano, Kati yetu kuna walio umia Viuno Mikono e.t.c kuna uharibifu wa Vifaa vyetu Vya kazi umetokea Pia, Wenzetu wanaendelea na Matibabu Mungu ni Mwema Mungu Ni Wetu Sote na Hili Nalo Litapita, Bado Tuna Wasiwasi Tu kama Mhusika ataendelea Kututafuta Ucku huu kwa ajili ya Kutudhuru Zaidi, Tunaskitishwa sana na Matumizi makubwa ya nguvu dhidi yetu sisi Wanyonge wa #Shilawadu
Kuna Watu watasema Shilawadu wamezidiiii na kusahau kuwa sisi Ni Wana Habari Kama Wana Habari Wengine
Na Kupata habari ni haki ya kila mwananchi kama ilivyo haki nyingine yoyote ile. Kifungu cha 18 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano 1977 na hatimaye kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 inampa haki mtu uhuru wa kujieleza na kutoa mawazo, uhuru wa kutafuta Habari, kupata Habari na kueneza habari bila kujali mipaka. Pia Sheria hiyo Inampa haki pia ya mtu kuwasiliana bila kubughudhiwa na mawasiliano hayo na kufahamishwa wakati wowote masuala yote muhimu yahusuyo maendeleo yake na yahusuyo jamii yake kwa ujumla
Na Muhojiwa Ana Haki ya Kukataa kufanya Mahojiano Hayo Au Kukataa Maudhui Hayo Yasiruke Hewani Kwasababu Jinsi Yanavyokusanywa sio Live
Taarifa zilizozagaa zinaeleza kuwa watangazaji wa kipindi hicho Soudy Brown na Kwisa wamepokea kipigo kutoka kwa dancer wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Moses Iyobo hapo jana wakati walipojaribu kumfanyia mahojiano kuhusiana na mzozo uliopo wa deni kati ya mpenzi wake Aunty Ezekiel na video vixer Tunda.
Bongo5