-->

Ishu ya Tunda, Aunt Ezekiel Iko Hivi!

AREMBO wa Bongo hawajawahi kuwa salama wala kumuacha mtu salama. Safari hii mambo ni moto kwelikweli kwa mastaa wawili wa kike, Aunt Ezekiel na Tunda.

Wadada hao wenye mvuto wa kipekee ndani ya Bongo, wamelianzisha kinoma huko kwenye mitandao ya kijamii na hali kwa sasa si shwari.

Ishu yao ilianza kama utani vile, lakini baadaye mambo yakaharibika zaidi baada ya kutoleana maneno ya shombo kwa siku kadhaa sasa.

Chanzo cha bifu hilo kinatajwa kuwa ni Tunda, ambaye amewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Young Dee, kudaiwa mkwanja ambao alitakiwa kulipia pombe alizokunywa.

Kwa mujibu wa Aunt Ezekiel, anadai Tunda ambaye ni mpambaji wa video za Bongo Fleva, anadaiwa Sh 100,000 za pombe alizochukua kwenye duka la demu huyo wa Moze Iyobo.

Hata hivyo, Tunda anadai kuwa alishalipa deni hilo, laki si pesa kama mashostito wa mjini wanavyoiita na alimkabidhi baba mtoto wa Anti, Iyobo ila haikufika kwa mhusika.

Lakini, wakati ishu nzima ya kudaiana ikiendelea kwenye mitandao, mara paap Iyobo ambaye ni densa wa WCB, aliibuka na kuposti picha ya Tunda kisha akashusha ujumbe wa shombo uliojaa matusi huku akimtetea mama watoto wake, Aunt Ezekiel.

Ujumbe huo ulizusha tafrani huko Instagram huku watu wengine wakimchamba kwa kuingilia mambo ya kike, ambapo Iyobo huenda kwa kushauriwa na watu wake alifuta fasta tu.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wataalamu wa kusambaza ubuyu mjini, imedaiwa kuwa wivu wa Aunt kwa Iyobo ndio umechangia tifu hilo dhidi ya Tunda.

Mara kadhaa Anti amekuwa akitemeana shombo na wenzake kwenye mitandao akiwatuhumu kumnyemelea Iyobo wakimtaka kimapenzi huku akichimba mkwara kuwa, wametoka mbali hivyo wamuachie mtu wake.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364