Tunda: Marafiki Wasiofaa, Utoto Viliniharibia Maisha
KABLA ya Video Queen Tunda Sabasita kukamatwa na polisi kwa soo la kutumia madawa ya kulevya kisha kufi kishwa mahakamani akiwa na mastaa wengine, alikuwa gumzo kutokana na matanuzi aliyokuwa akiyafanya kwenye mahoteli makubwa kisha kutupia picha kwenye mitandao.
Wengi walihoji kama kweli ni sanaa tu ambayo inamuweka mjini au kuna madili mengine lakini majibu hayakupatikana. Pia ukizungumzia mamodo ambao huvaa vivazi vya nusu utupu, ‘mtoto’ huyu yumo.
Hata hivyo, baada ya msala wa madawa ya kulevya, amekauka kwenye mitandao na hata zile vurugu alizokuwa akifanya zimeyeyuka. Ijumaa lilitaka kujua maisha yake kwa sasa yakoje na ndipo lilipomtafuta na kufanya naye mahojiano;
Ijumaa: Mbona umepotea sana mdada, kulikoni?
Tunda: Nipo jamani ila sasa hivi nimeamua tu kubadilisha mfumo mzima wa maisha yangu maana nimebaini nilikokuwa naelekea hakukuwa sahihi.
Ijumaa: Umebadilika kivipi?
Tunda: Kwanza nimepunguza mashoga wasioeleweka maana nimebaini watanipoteza. Lakini pia nimejiondoa kwenye mitandao ya kijamii tofauti na nilivyokuwa zamani.
TUNDA: Kiukweli siko na Young D tena, sasa hivi nina mpenzi mwingine kabisa, na nahisi huyu ndiye atakuwa mume wa maisha yangu muda utakapofi ka
Ijumaa: Umejiondoa kivipi?
Tunda: Ni kwamba sizingatii tena kama zamani kwamba kila siku lazima nipige mapicha nikila bata zangu kisha niweke huko, au kufuatilia kwa ukaribu vitu vya mtandao, siku hizi hakuna hiyo. Ijumaa: Nini kilikufanya uamue hivyo?
Tunda: Nilihitaji kubadilika kabisa na watu wanione tofauti na nilitaka kuwa kidadadada zaidi, utoto niweke pembeni.
Ijumaa: Kipindi ulipopata skendo ya utumiaji wa madawa ya kulevya familia yako ilikuchukuliaje?
Tunda: Hivi ndugu zako wapate habari kama hizo halafu wachukulie poa, inawezekana kweli? Kiukweli waliumia sana lakini yamepita.
Ijumaa: Umejifunza nini kupitia hilo?
Tunda: Nimejifunza kuchagua marafiki wa kuwa nao maana inawezekana wao ndiyo walikuwa sababu ya kupotea kwangu.
Ijumaa: Vipi kuhusu uhusiano wako na Young D, maana mara tusikie mmeachana, mara mmerudiana, hebu tupe ukweli.
Tunda: Kiukweli siko na Young D tena, sasa hivi nina mpenzi mwingine kabisa, nahisi huyu ndiye atakuwa mume wa maisha yangu muda utakapofika.
Ijumaa: Inadaiwa kuwa, sasa hivi una mimba, nalo likoje hili?
Tunda: Ni kweli lakini bado ni changa na kiukweli namuomba Mungu nizae maana nahisi nikiitwa mama nitatulia zaidi.
Ijumaa: Utakuwa tayari kutulia na kulea mtoto wako kweli?
Tunda: Na tena mimi nitakuwa mama wa mfano kwa mastaa wote waliotangulia kuzaa.
Ijumaa: Hivi umodo ndiyo unakulipa na kukuwezesha kufanya matanuzi kama tunayoyaona kwenye mitandao ya kijamii?
Tunda: Kwanza mimi sifanyi U-video Queen kwa ajili ya pesa, sawa nalipwa lakini siyo kivile. Umodo ni kazi ninayopenda tu kutoka moyoni.
Ijumaa: Sasa unapata wapi pesa za matanuzi vile?
Tunda: Mjini mbona kuna vitu vingi sana vya kufanya halafu siyo vizuri kuviweka wazi kila mtu akajua.
Chanzo;GPL