-->

Uchebe Afungukia ‘Honeymoon’ Yake na Shilole

Mume mtarajiwa wa msanii ambaye ni mfano wa kuigwa kwa mabinti kutokana na juhudi zake za kupambana na maisha, Zuwena Mohamedi au Shilole, ameweka wazi matarajio ya kumpeleka Ulaya kula ‘honey moon’ mke wake huyo mtarajiwa.

Uchebe na Shilole

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, mwanaume huyo anayejulikana kwa jina la Uchebe, amesema ndoa yake na msanii huyo itakuwa mwezi wa 12 mwaka huu kwa kuwa ameshakamilisha taratibu zote za kuhalalisha mahusiano yake na msanii huyo.

“Mwenyezi Mungu afanyie wepesi sasa hivi tupo kwenye maandalizi, na akipenda mwezi wa 12 itakuwa ndoa kwani taratibu zote nishafuata, mahari mi nishamaliza sidaiwi, na honey moon nampeleka Ulaya”, amesema Uchebe ambaye ndiye shemeji yetu kwa Shilole.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kwamba wawili hao wameachana, na Shilole kukanusha taarifa hizo na kusema kwamba wawili hao bado wapo pamoja.

Fahamu kwamba pamoja na vituko vyake vingi, Shilole ni mfano bora kwa mabinti kutokana na bidii anazoonyesha kwenye kupambana na maisha, ambapo mpaka sasa ni mjasiriamali mkubwa, kwa kuwa na mgahawa wa chakula, bidhaa ambayo ni brand yake pamoja na kusimamia wasanii wengine.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364