-->

Ujauzito Feki wa Nisha Wamsababishia Haya

Mcheza filamu maarufu katika soko la filamu Bongo Movie, Salma Jabu, maarufu kama Nisha Bebee amejipotezea uaminifu mtaani anapoishi na jamii nzima inayomzunguka kwa kitendo cha kuudanganya umma mwishoni mwa mwaka 2016.

Nisha

Nisha aliibuka na kudai kuwa ni mjamzito na ujauzito huo aliupata kutoka kwa mmoja wa wasanii wa Bongo Fleva kwa kubakwa. Habari ya ujauzito wa Nisha ilipata mashiko kwa jamii kwani ilithibitishwa na Nisha mwenyewe katika mahojiano katika kipindi cha XXL cha Clouds FM mwisho mwa mwaka jana.

Wakazi jijini Dar es Salaam wamedai ya kwamba kitendo alichofanya Nisha si sahihi kwani huwezi kuudanganya umma kwa jambo kubwa kama hilo la ujauzito. Wakati Nisha anakanusha kuwa hakuwa mjamzito ingetokea taarifa za kutupwa mtoto sehemu basi jamii ingejua wazi Nisha ndiye aliyetupa mtoto.

Nisha

Hivyo kwa jambo hilo si busara na pia ni hatari sana kutafuta umaarufu kwa njia za udanganyifu. Kwa sasa Nisha anaonekana kama muigizaji tu hata katika maisha halisi. Mfano akifika msibani anaonekana kama amefika kuigiza tu wala si hashiriki shughuli za kijamii.

Salum Milongo/GPL.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364