-->

Ukiwa Staa Unatafuta Marafiki wa Faida – Gabo

NYOTA wa filamu Bongo Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ amesema kuwa kwa mtu anayetazama mbele kila hatua anayopiga ili asonge mbele lazima abadilishe marafiki kufikia ndoto zake na kama itatokea mtu akabaki na kuendelea na marafiki wa awali hatofanikiwa katika harakati zake.

“Kuna wakati watu wengi hukosea kuishi kwa mazoea unaweza kusikia kuwa Gabo alikuwa rafiki yetu siku hizi kabadilika ana marafiki wapya sasa unakuweje na rafiki ambaye anataka muda wote mpo maskani tu,”

Gabo anasema kuwa maisha ya sasa ni mbio inatakiwa vijana wengi wasitumie muda wao kuwa na marafiki ambao hawana ushauri wa kimaendeleo kwani ni rahisi kutengeneza Taifa la omba omba wakati kuna vitu vingi vya kufanya na kuendesha maisha bila kuwa tegemezi.

Anaamini hakuna miujiza katika kutafuta hasa kwa kuchagua marafiki wanaofikiria jinsi ya kufanya kazi na si vinginievyo maana muda si rafiki katika utafutaji ukibaki nyuma unapotea kwa sababu tu ya kuhofia utawaacha rafiki zako.

Filamucentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364