-->

Aunt Ezekiel Afungukia Ukimya Wake

Muigizaji mahiri kutoka bongo, Aunty Ezekel amekiri kuwa suala la yeye kuingia kwenye suala zima la malezi ndiyo chanzo cha ukimya wake na kubainisha kuwa kwani kipindi hicho ndiyo wakati ule mauzo ya soko la filamu yaliporomoka nchini.

Aunty Ezekel

Akizungumza kwenye zulia jekundu mapema wiki hii katika uzinduzi wa filamu ya muigizaji mwenzake Wema Sepetu, Aunt amesema hakuwa na uwezo wa kutoa filamu kipindi alipoingia kwenye malezi kwani soko lilikuwa haliridhishi.

“Umama umenikuta katika kipindi ambacho soko la ‘movie’ lime-drop, lakini ndani ya umama huo imenipa muda wa kufikiria na kufanya kazi nzuri zaidi. Hivyo nategemea kufanya makubwa siku za karibuni nikijaaliwa uzima, lakini hichi alichokifanya Wema ni kitu kikubwa sana kwenye tasnia” Aunt.

Akizungumzia kuhusu ukaribu wake kupungua kati ya yeye na muigizaji Wema, Aunty amefunguka na kusema kuwa yeye kuwa na familia ndiyo chanzo kwani muda mrefu anakuwa na familia.

“Siyo kwamba hatuna mahusiano mazuri, ni kwamba mimi sasa hivi naishi na familia muda mwingi nipo na familia tofauti na mwenzangu ambaye yeye bado anaishi peke yake kwa hiyo ndiyo sababu ya sisi kutokuonekana pamoja lakini siyo kwamba kuna kitu kibaya kinaendelea kati yetu sisi” Aunt.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364