-->

‘Upcoming’ Wameharibu Soko la Bongo Movie – Sandra

Mkongwe wa bongo movie Sandra amewachana wasanii wanaoingia katika tasinia ya bongo movie kwa malengo ya kupata umaarufu ili wapate njia za kufanya mambo yasiyofaa katika jamii kupitia umaarufu walioupata.

sandra

Sandra – Msanii wa Bongo Movie

Akiongea ndani ya eNewz Sandra amesema watu wanaopata skendo mbaya kupitia umaarufu walioupata ndani ya bongo movie wanasababisha kupoteza heshima za wasanii wanaojiheshimu lakini pia inaharibu tasnia nzima ya bongo movie na kunyima ajira wasanii wengine.

Hata hivyo Sandra amewasihi na kuwashauri waandaaji wa bongo movie kuangalia watu wa kuwaweka katika movie lakini pia amewasihi wasanii wanaoingia katika tasinia wachague sehemu ambazo zinamfaa kuigiza ili kuweza kurudisha soko la bongo movie na kuwafurahisha mashabiki

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364