-->

Usharobaro Wamtokea Puani Stan Bakora

STAN BAKORA

Usharobaro umemtokea puani komediani wa Bongo, Stanley Yusuph ‘Stan Bakora’ baada ya kudondoka na kuumia mguu wa kulia wakati akifanya mazoezi ya kutumia Cyboard (Saibodi).

Ishu nzima ilitokea wiki iliyopita katika moja ya duka la nguo lililopo Kinondoni, Dar baada ya kupiga mwereka wa kufa mtu na kujikuta akianguka kama mkungu wa ndizi kutoka juu ya mgomba kisha kuumia mguu.

Akiwa kwenye Cyboard

Akiwa kwenye Cyboard

“Hicho kidude, kwangu ni kigeni ndiyo nilikuwa nakijaribisha nione inakuwaje ndipo nilipoanguka kama mara mbili hivi na kuumia mguu wa kulia, kiukweli kimenitoa ushamba,” alisema Stan Bakola.

Chanzo:GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364