-->

Nilimpokea Sharomilionea kwa Mikono Miwili-Kitale

Msanii wa vichekesho Kitale alimaarufu kama Mkude Simba amefunguka na kusema kuwa yeye ndie aliyempokea aliyekuwa msanii wa vichekesho na msanii wa bongo fleva marehemu Sharo Milionea.

KITALE

Akipiga stori katika kipindi cha Mkasi Tv kinachorushwa kupitia ting’a namba moja kwa vijana (EATV) Kitale amesema kuwa yeye ndiye alimpokea Sharo Milionea na kumtambulisha kwenye tasnia, Kitale alidai wakati Sharo Milione amekuja katika kikundi ambacho na yeye alikuwepo kuna watu walimkataa kabisa Sharo Milionea lakini yeye na Sharo Milionea ilitokea damu zao kupatana.

“Unajua wakati Sharo Milionea anakuja kwenye kikundi ambacho nilikuwepo kuna watu walimkataa kabisa Sharo Milionea na hao ndio watu ambao walikuwa wanasimamia kazi ambayo tulitakiwa kufanya, lakini Sharo Milionea alikuwa ananiambia anatamani kuwa kama mimi, hivyo sikupenda kuona anafanyiwa vile hivyo nakumbuka baada ya hapo niliamua kuachana nao na baada ya kuachana nao nilikaa siku kama tatu nikapigiwa simu na Mzee Majuto na kuniambia kuna don mmoja anataka wasanii wa Comedy ndio hapo niliamua kumchukua na Sharo Milionea na kwenda nae” Alisema Kitale

Katika hatua nyingine Kitale amesema siku ambayo Sharo Milionea anakwenda Tanga na kupata ajali iliyopelekea kifo chake alikuwa akitaka waende pamoja lakini yeye alishindwa kwenda sababu alikuwa anaumwa.

“Unajua siku ile alinipigia simu na kuniambia yupo Ubungo mataa na mimi nilikuwepo maeneo hayo lakini nikamuuliza upo Ubungo kweli maana sikuoni ndipo hapo alitoa kichwa kwenye gari aina ya Harrier na kuanza kuongea zile swaga zake hivyo nilimuona, lakini baadaye akanipigia simu na kunieleza amepaki gari maeneo ya Ubungo maji lakini kwa kuwa nilikuwa naumwa nilishindwa kuonana nae, kiukweli siku ile yeye alikuwa ananipigia simu akiwa na furaha sana lakini mimi sikuwa na raha kabisa, nakumbuka nilikuwa nimelala simu yangu ikawa inaita tena kuangalia naona ni yeye nilipopokea simu akaniambia yupo Chalinze ndio anaelekea Tanga, nakumbuka baadae nilipopigiwa simu nikaona ni yeye tena kupokea simu mtu akaniuliza tu wewe Kitale? nikamwambie ndio akaniambia mtu mwenye simu hii amefariki kwa ajali ya gari, kiukweli siku amini na muda huo huo nilipona, baadae nikapigiwa simu na Tunda Man na kupewa taarifa kama hiyo hiyo ila bado sikuamini, ila aliponipigia simu mjomba na kuniambia ndio niliamimi na muda huo huo nilipoteza kumbukumbu” Amesema Kitale

Eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364