-->

Utata: Tunda Man Afunguka Juu ya Miujiza ya Ajali Yao

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Tunda Man, ameamua kuadithia mkasa mzima uliotokea kwenye ajali waliyoipata weekend iliyopita Mkoani Iringa na kusababisha kifo cha msanii mwenzao Man Katunzo.

Tundaman32

Tunda Man

Akizungumza na Enewz Tunda Man amesema, “Wakati tupo njiani marehemu aliniita katika gari yake nikahama katika gari niliyokuwa nimepanda na kuhamia katika gari yake na wakati huo wote aliokuwanao mpaka ajali inatokea walikuwa wamelala”.

Enewz ikazungumza na mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo muongozaji wa Video za Bongo Fleva Marijani ambaye alikana uwepo wa Tunda Man katika gari iliyopata ajali na kusema kuwa Tunda hakuwa katika gari hiyo, bali gari iliyokuwa nyuma yao.

Kuhusu tuhuma dhidi ya mwanamuziki huyo kuiba vitu vya marehemu vilivyokuja kupatikana katika gari yao wakati wanasachiwa katika kizuizi cha mikumi mkoani Morogoro, Tunda alikana kufanya tukio hilo na kudai kuwa vitu hivyo alipatiwa na ndugu wa marehemu kwaajili ya kuvihifadhi.

Polisi mkoani Iringa ACP Peter Kakamba amethibitisha uwepo wa ajali hiyo na kumjumuisha Tunda katika gari iliyopata ajali na kwamba majeruhi wote wanaendelea vizuri

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364