Utumbuaji Majipu Sasa Watua Kariakoo kwa Wezi wa Filamu
UNAPOSEMA Serikali ya awamu ya tano ilichoahidi lazima kifanyike ni kweli kabisa hivi karibu Mh. Nape Moses Nnauye alisema kuwa atahakikisha kuwa wale wanaojipatia fedha kwa njia za ujanja ujanja mwisho wao umefika lazima washughulikiwe kulinda maslahi ya Wasanii wa Tanzania.
Jana ilikuwa ni siku mbaya kwa wale wauuzaji wa filamu za nje baada ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kutinga na Polisi kwa muuzaji mkubwa wa Dvd Fake Kariakoo mwenye mtaji mkubwa ajulika naye kwa jina la Palasi na kukamata kazi fake zote na kuzipakia katika Gari.
Tajiri huyo aliyetajwa kwa jina la Phili Ulaya Mdalo almaarufu kama Palasi alikutwa na balaa hilo na kukutwa na mzigo wenye thamani ya milioni 80 na mashine 5 za kurudufu kazi bandia za nje na ndani huku ikisemekana ndio mmiliki wa Butterfly Hotel zilipokamatwa Fake hizo.
‘’Mali tulizokamata kutoka kwa mfanyabishara huyu nipamoja na Cd pamoja na Dvd ambazo ni kazi za wasanii mbalimbali wakutoka nje na ndani ya nchi, ‘’alisema Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi TRA Richard Kayombo .
Zaidi ya maduka 70 yamefungwa ambayo ndio vinara wa kuuza sinema hizo bandia kutoka nje huku wakiwa wamebandika maneno makali kwa serikali na wasanii wa filamu Swahilihood lakini ukweli ni kwamba wizi hauingiliani na ubora wa kazi ya mtu mwingine .
Jana tu kuanza kwa zoezi hilo tayari mauzo ya filamu yameanza kupanda sana kwa filamu za ndani jambo ambalo linaonyesha wazi kulikuwa na ubanaji wa kazi za ndani Serikali inahitaji kupongezwa kwa hilo kwani filamu ndio sekta yenye uwezo mkubwa wa kutoa ajira.
FC