Picha: Diamond Akutana na Kanye West Marekani
Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameshare picha akiwa na mkali wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Kanye West. Diamond alisafiri kuelekea Marekani Las Vegas kwa ajili ya kufanya show, ambapo kwenye maelezo ya hii picha, ilionekana wakati huo alikuwa Los Angeles.