-->

Uwoya: Nasaka Pesa Kwa Sababu ya Mtoto Wangu

STAA wa filamu za Bongo Movie, Irene Uwoya, ameweka wazi kwamba bidii yake na ubunifu aliouongeza katika kazi zake anazofanya kwa sasa zinatokana na nia yake ya kutaka kumwandalia mazingira bora mtoto wake, Krish.

Uwoya alisema kwa sasa anaweza kukidhi mahitaji yote ya mwanae lakini hatayamudu kama hataendeleza ubunifu katika sanaa ya uigizaji na shughuli zake nyingine.

“Unajua kadiri mtoto anavyokua mahitaji yanaongezeka, ndiyo maana kila ninapomkumbuka nahisi nina deni kubwa la kumwandalia maisha bora mwanangu,” alieleza Uwoya.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364