Uzinduzi wa Tanzanite International Film Festival
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye Jumapili hii mkoani Arusha amezindua tamasha kubwa la Kimataifa la Filamu, ‘Tanzanite International Film Festiva’.
Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa filamu waliohudhuria uzinduzi wa tamasha hilo, kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja.
Tamasha hilo litakuwa chachu kwa tasnia ya filamu Tanzania kwa kuwa ni kwa muda mrefu walikosa matamasha ya namna hiyo ambayo husaidi kutangaza filamu.
Bongo5