Diamond Afungukia ‘Reality Show’ Yake, Kuonekana kwa Njia Hizi
Inawezekana wasanii wakubwa kutoka nchini Nigeria, P.Square ambao sasa hivi wako nchini South Africa wakishoot video ya ngoma mpya ya Diamond wakaonekana kwenye ‘reality show’ ya huyo ambayo itaanza kuonekana hivi karibuni,kwenye moja ya post zake kwenye page yake ya ‘Instagram’ aliandika kuwa shoo hiyo sio ‘kireality show’ bali ni ‘reality show’.
‘’Nikisema sio kireality ina maana kwamba sio tu bora reality,watu wamekuwa wakisubiria kwa muda mrefu mbali na hivyo pia hata mimi nilikuwa natamani kufanya muda mrefu lakini nilikuwa nataka vitu vikamilike kama production kwa sababu ukizungumzia reality unazungumzia production kuwe na vifaa bora, kuwa na content za kutosha sasa uzuri mie mwenyewe ‘content’ ninazo kwa sababu kila siku nasafiri nina matukio mengi sana na vitu vingi sana kwahiyo na kupata sponsor ambaye ni mkubwa amabye anaweza kuingiza hela nyingi inatakiwa iwe imecreatiwa vizuri na kila kitu, kwa sasa kila kitu kiko sawa,kwahiyo katika step za mwisho ili kitu kipakuliwe itakuwa online na kwenye tv lakini exclusive zitaanzia katika moja ya mtandao halafu ndio inaingia kwenye kipindi labda wiki inayofuata’’Alisema Diamond.
Cloudsfm.com