-->

Vanessa Atokwa Povu Kuambiwa Anajichubua

Ubuyu unaotrendi Bongo unamgusa staa wa Bongo Fleva anayekamata anga za kimataifa, Vanessa Mdee ‘V-Money’ ambaye wikiendi iliyopita alitawala mitandao ya kijamii kwa picha yake iliyomuonesha akiwa amevaa kibukta na kuachia maungo yake wazi kisha mashabiki wakahoji kuwa rangi ya maungo haifanani na rangi ya uso wake ‘eti baadhi ya sehemu amekunywa maji mengi’.

vanessa33

Vanessa Mdee ‘V-Money’

Mwana-ubuyu wetu alipoona picha hiyo imefunika mitandaoni, aliamua kuangaza kwenye kila akaunti ambapo alikutana na komenti nyingi zilizoonesha madai kuwa mwanadada huyo, kuna wakati huwa anaediti sura yake na kuonekana mweupe na kuna wakati anakuwa na ngozi ya maji ya kunde.

Hata hivyo, wapo waliomvaa jumlajumla wakidai amekuwa akitumia mkorogo na kusahau baadhi ya maungo lakini pia wapo waliodai kuwa ni picha za Instagram ambazo mtu ana uwezo wa kuzifanya zikang’aa na akaonekana apendavyo.

“Picha za mtandaoni ni noma! Unaweza ukadhani kitu kimetoka Ulaya leoleo lakini ukikutana nacho laivu, utajiuliza mara mbilimbili. Hicho ndicho kinachotokea kwa akina dada walio wengi wanaopenda kuuza sura,” alisema Antonio, mmoja wa wachangiaji mtandaoni.

Baada ya Wikienda kuona ishu ya Vanessa imekuwa gumzo kutokana na komenti hizo ndipo likajiongeza na kuufanyia kazi ubuyu huo kwa kutafuta ukweli kwani mbali na rangi ya ngozi, pia wapo waliomdisi kimavazi lakini pia wapo waliompongeza kwa kwenda na wakati wakidai kuwa anavaa kimataifa zaidi. Wikienda kama kawaida yake lilimsaka Vanessa ili kumfikishia tuhuma zake za kujiediti na kutumia mkorogo.

VANESSA ATOKWA POVU 
Katika kumtafuta Vanessa ili kuzungumzia kile kilichotrendi mtandaoni, Wikienda lilimwendea hewani kupitia simu yake ya mkononi kwani hakuwepo Dar badala yake ilielezwa kwamba yupo nchini Kenya akirekodi na mwanamuziki mkubwa wa Marekani, Trey Songz. Intavyu ya Vanessa na Wikienda ilikuwa hivi;

Wikienda: Vanessa mambo vipi? Kuna maswali kadhaa nataka kukuuliza, uko free tuchati?

Vanessa: Oke.

Wikienda: Kuna picha zipo mtandaoni umebebwa stejini, mashabiki wako wanasema make-up zinakusaidia na wengine wanadai unajichubua usoni tu, mwilini umeusahau! Je, wewe unaliongeleaje hilo?

Vanessa: Unadhani swali lako linanijenga nini mimi? Nakuomba uchunguze maswali yako kabla ya kuniuliza.

Wikienda: Swali lina maana kubwa, wewe ni kioo cha jamii, kwa kuwekwa mtandaoni na kujadiliwa kuwa unajichubua, huoni kama unachafuliwa? Kwangu mimi nimeona nikupe nafasi ya kufunguka huenda kuna watu wanataka kukuharibia.

Vannesa: Kwa sasa niko Kenya, nafanya kazi na msanii mkubwa wa Kimarekani, Trey Songz hujaandika lakini unataka kuniuliza maswali ya ajabu tu, kweli hayo ni maendeleo?

Wikienda: Kazi yangu ni kuuliza kila kitu kama nakiona hakiendi sawa hasa kwa mastaa kutokana na gazeti ninaloliandikia, wewe jibu tu kwani nimekupa nafasi.

Vannesa: Umenikwaza, naomba tuachane kwa sasa!

Baada ya kuachana na Vanessa, kumbe alimpatia meneja wake namba ya mwandishi wetu ambaye alimtafuta Mwana-ubuyu kwa ajili ya kuweka mambo sawa ambapo naye alifunguka kama hivi.

Meneja: Naitwa Tommy kwa jina. Ni meneja wa Vanessa, naomba tuwasiliane tafadhali.

Wikienda: Poa una jipya lipi? Naona mmepaniki mpaka wewe umenipigia.

Meneja: Yaah! Nimeona maswali unayomuuliza Vannesa, naona kama unauliza kabla ya kuchunguza nadhani kazi yako inakutaka kuwa makini kwanza.

Wikienda: Mimi niko makini sana ila ninyi mmepaniki, staa hatakiwi kupaniki, anatakiwa kujibu kile anachoulizwa tu.

Meneja: Oke! Mimi ndiye msemaji wa mwisho wa Vanessa, niulize nitakujibu.

Wikienda: Kuna madai kuwa msanii wako anajichubua kwa sababu kuna picha imetrendi akiwa stejini na mwanaume, maungo yake yanaonekana kuwa meusi wakati usoni ni mweupe, je, unaweza kulijibu hilo?

Meneja: Kwanza nikurekebishe, yule mwanaume ni Jux, lakini Vanessa hajichubui, anaipenda ngozi yake na nikwambie tu kwenye ulimwengu wa kisasa, Smart Phones zinatofautiana na inawezekana picha zinakuwa na ubora tofauti kutokana na kamera za simu kwani utakuta huyu anatumia Tecno, mwingine anatumia Iphone, lazima ubora wake utakuwa tofauti. “Tunaona kila kitu kinachoandikwa mtandaoni na siyo kila action inatakiwa kuwa na reaction.

Sometimes ukikaa kimya pia nalo nijibu. Wewe unajua tupo kwenye karne gani. Smart phones ni nyingi na kila simu ina uwezo wa kamera yake. “Huwezi kumzuia shabiki, hata akiwa na aina yoyote ya simu, akitaka kupiga picha na Vanessa, nitaruhusu tu.

“Kwa hiyo, quality ya picha iliopigwa na kamera ya shabiki wa Vanessa haikuwa sawa na wala siyo kwamba anajichubua,” alifunguka meneja huyo.
Alimalizia: “Vanessa anapenda ngozi yake na hana sababu ya kujichubua. She is comfortable in her skin aliyozaliwa nayo.”

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364