Vanessa Yuko Kipesa Zaidi na Sio Mapenzi!
Msanii Vanessa Mdee amefunguka ya moyoni na kusema kuwa kwake pesa ndio kila kitu, na sio mapenzi ya kweli.
Kwenye kipindi cha Friday Night Live ambacho kinarushwa na East Africa Television na East Africa Radio, Vanessa ametoa jibu kuwa yeye anapenda pesa zaidi, kuliko mapenzi, na kuibua hisia kuwa huenda hata kwa mwandani wa ambaye pia ni msanii anayefanya poa kwenye bongo Fleva Juma Jux, yupo kipesa zaidi na si Mapenzi.
Mtangazaji wa kipindi hiko alisikika akimuuliza vanessa maswali ambayo alitakiwa kujibu ndani ya sekunde, na ndipo alipotoa jibu hilo kuwa anapenda pesa zaidi.
Sam: Unachukua muda gani kuvaa getting ready?
Vanessa: 30 minutes
Sam: Diamond au pulse?
Vanessa: Diamond
Sam: Hils au sneakers?
Vanessa: Sneakers
Sam:Dresses au trousers?
Vanessa:Trouser
Sam: Icecream au chocolate?
Vanessa:Chocolate
Sam:Nyama au Salad?
Vanessa:Nyama
Sam: Diamond au Alikiba?
Vanessa: Vanessa
Sam: Bags au purses?
Vanessa: Bags
Sam: Ugali au wali?
Vanessa: Ugali
Sam: Mapenzi au pesa?
Vanessa: Pesa
Pia katika maswali hayo Vannesa Mdee alishindwa kuweka wasi ni msanii yupi anamkubali zaidi kati ya Diamond na Alikiba, baada ya kuulizwa kuhusu wao na kuamua kujitaja mwenyewe.
Eatv.tv