-->

VIDEO: Jay Moe Amtetea ‘Mamu’

Mkongwe ambaye bado anaonesha ubabe wake kwenye game Juma Mchopanga ‘ Jay Moe’ amtetea aliyekuwa msambazaji wa albamu za muziki wa bongo ‘Mamu’ na kusema kuwa hakuwahi kuwanyonya wasanii kama jinsi watu wanavyodai bali wezi walimzidi ujanja.

Akizungumza kupitia eNewz ya EATV, Jay Moe amedai kuwa msambazaji huyo alizidiwa ujanja na baadhi ya maharamia wa kjazi ya sanaa ambao walikuwa wakitafuta ‘Masta’ moja tuu kisha wanaanza kuuza kinyamera pasipo mamu kujua jambo ambalo lilikuwa likimfanya ‘Mamu’ kupambana nao kwa kila njia.

“Unajua wakati ‘Mamu’ analalamikiwa kwamba anawaibia wasanii, yeye pia alikuwa akilalamika kuwa anaibiwa ndiyo maana hata nakala zetu tulizokuwa tunaziuza yeye alikuwa anataka ‘stamp’ za kila msanii ili aweze kupambana na wale maharamia na hata mtaani tulikuwa tunazikagua tukikutana na wamachinga kwa hiyo siyo kweli kama alikuwa anatunyonya maana wapo wasanii wengi waliowahi kufaidika na uwepo wake kama kina Ferooz, Prof Jay, Juma Nature na wengine” – Jay Moe alifunguka.

Pamoja na hayo Jay Moe amefunguka na kuongeza kuwa “Kelele za wasanii kuhisi kwamba wanaibiwa na muhindi huyo ndio chanzo kuachana na uuzaji wa albamu lakini pia muhindi huyo kushindwa kuendana na utandawazi ndicho kilichomfelisha katika suala la kuendelea kuuza albamu” Jay Moe

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364