Wema Sepetu Apandishwa Tena Kizimbani Kisutu Leo
Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na wenzake wawili, Matilda Abass na Angelina Msigwa ambao ni wafanyakazi wake wa ndani kwa kosa la matumizi na kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi lakini amekana mashitaka hayo yote.
Mahakama imeahirisha kesi yake hiyo na itasikilizwa tena Julai 14, mwaka huu.
Chanzo:GPL