-->

Wolper Ataja Vitu Anavyovikumbuka kwa Alikiba

Msanii wa filamu Bongo Jackline Wolper amefunguka mengi kuhusu Alikiba ambaye alikuwa mpenzi wake.

Wolper amedai kuwa anakumbuka mambo mengi kutoka kwa mpenzi wake huyo, zaidi akikumbuka upole wake pamoja na unyenyekevu.

“Mengi nakumbuka, kikubwa ni upole wake pamoja na unyenyekevu. Ni tofauti na wanaume wengine ambao nimewahi kukutana nao,” muigizaji huyo ameliambia gazeti la Amani.

Kwa sasa Wolper ameonekana kuwa mwenyewe japo hajaweka wazi tangu alipotoa taarifa za kuachana na Harmonize ambaye amekuwa na mahusiano naye ya kimapenzi tangu mwaka jana alipoachana na Mkongoman wake.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364