VIDEO: Kwanini Mzee wa Upako Anamkubali JPM?
Mchungaji Anthony Lusekelo wa Kanisa la Maombezi Ubungo KIbangu, ameelzwa kukunwa na utendaji wa serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais John Magufuli, huku akiweka wazi asili ya jina lake la ‘Mzee wa Upako’
Akiwa katika kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, Mzee wa Upako alitaja baadhi ya mambo yanayomfanya aikubali na kuridhika na serikali hii kuwa ni pamoja na mikakati ya kuondoa wafanyakazi hewa, ununuzi wa ndege, nidhamu katika utumishi, ujenzi wa treni ya umeme, n.k
Kitu kingine alichoeleza kukikubali zaidi ni uamuzi wa serikali hiyo kulazimisha kampuni za mitandao ya simu, kuuza hisa zaidi katika soko la hisa, ili kila mtanzaia apate fursa ya kushiriki uchumi wa nchi.
Pia Mzee wa Upako amezungumzia umuhimu wa taifa kuweka mazingira ya haki kwa kila raia, kwa kuwa haki ndiyo inayofanya amani iwepo, na penye amani ndipo kwenye maendeleo, hivyo Tanzania haiwezi kuwa na maendeleo kama hakuna haki.
“Mahali popote ambapo hakuna haki basi hakuna amani, amani ni matokeo ya haki, na penye amani ndipo penye maendeleo” Alisisitiza Mzee wa Rais Magufuli