-->

“Video Queens’ Wanataka Umaarufu si Pesa – Wadau

KIDOA34

Hayo yameelezwa na wadau mbali mbali walipokuwa wakitoa maoni yao kuhusu wasichana wanaofanya kazi hiyo kwenye kipindi cha PlanetBongo kinachorushwa na East Africa Radio.

“Mi naitwa Abduli naishi mwenge, kwangu mimi ninavyojua video models bongo kwa malipo hawalipwi vile wanavyopaswa, ila wanachokifaidi ni umaarufu kwa hiyo unakuta mtu anajitolea kufanya kazi na msanii fulani kwa sababu ya umaarufu, anajua kupitia umaarufu may be atatoka kisanaa kama muigizaji au kitu kingine, lakini kwenye malipo hawalipwi kama vile wanavyolipa”.

Kutokana na hali hiyo wadau hao wameshauri kuwa na mawakala maalum wa kupitia ili kuweza kuwapata video models, itakayorahisisha na kuwapa malipo mazuri.

“Mi nadhani kama mtu akitaka models, apitie kampuni fulani ama sehemu fulani, kwa hiyo mtu anajua naweza kuwa model wa kitu fulani awe katika kampuni, kwa hiyo mtu kama msanii akienda katika hiyo kampuni anampata mtu fulani inakuwa simple”, alisema mdau huyo”, alisema Abduli

Pamoja na hayo wasichana hao wametakiwa kufanya bidii katika kazi zao, ili kuweza kuipa thamani na hatimaye kuwalipa vizuri.

“ukifanya kazi mbovu utaonekana wewe hauna thamani ya hiyo kazi, cha msingi wao wajitahidi kwenye kazi zao, waonyeshe kipaji chao sio wakae tu wabweteke”, alisema mdau mmoja aliyejulikana kwa jina la Fadhili.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364