-->

VIDEO: Ronaldinho ametangaza kustaafu, jikumbushe vitu vyake uwanjani

soka wa kimataifa wa Brazil Ronaldinho Gaucho leo ametangaza rasmi kustaa kucheza soka la ushindani baada ya kudumu katika soka la ushindani kwa zaidi ya miaka 15, Ronaldinho amefikia maamuzi hayo baada ya kucheza soka kwa muda mrefu na sasa anaamini inatosha.

Ronaldinho hadi anatangaza kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 37, amecheza vilabu zaidi ya saba toka aanze kucheza soka vikiwemo vilabu vya Paris Saint Germain ya Ufaransa, FC Barcelona na AC Milan.

Kama hufahamu Ronaldinho alizaliwa mwaka March 21 1980 Porto Alegre kwao Brazil na alinza kucheza soka katika timu ya vijana ya Gremio 1987, jina lake halisi ni Ronaldo lakini aliitwa Ronaldinho kutokana na kuwa na umbo dogo kuliko wote katika timu ya vijana aliyokuwa anacheza wakati huo akiwa na umri wa miaka 8.

Ronaldinho alianza kuingia kwenye headlines za vyombo vya habari akiwa na umri wa miaka 13, hiyo ni baada ya kufanikiwa kuipatia ushindi timu yake wa magoli 23-0 lakini magoli yote 23 alifunga yeye, hivyo nyota yake ya kuja kuwa staa wengi wanaamini walianza kuiona mapema.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364