-->

VIDEO: Simgandi Mume Wangu – Riyama

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Riyama Ally amekanusha zile tetesi za yeye kumganda mume wake kwa wivu mpaka katika kazi zake anazozifanya za kimuziki na kudai yeye aliombwa kufanya hivyo.

 

 

Riyama amebainisha hayo baada ya watu kumuona katika video ya muziki ya msanii wa bongo fleva Leo Mysterio ambaye ndiyo mume wake huku wakidai kuwa wivu wa Riyama ndiyo umempelekea mpaka kuwa video quen katika nyimbo hiyo.

“Aliyeshauri ni mwenyewe Mr. Leo Mysterio, alisema mimi ndiyo nataka wewe uwe ‘video quen’ nikamwambia hapana, mbona wapo wasichana wazuri wengi tuwachukue wanaojulikana na wasiojulikana na wapo kwa ajili ya kazi hii akasema hapana huu wimbo una stori na unakuhusu wewe, basi na mimi nikaangalia nikaona video kweli inani hitaji”, alisema Riyama.

Pamoja na hayo, Riyama amesema hawezi kuwaogopa video ‘queen’ kwa kuwa wao ni wanawake na yeye ni mwanamke.

EAT.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364