-->

VIDEO: Sina Mpango wa Kubadili Jina – Harmorapa

Msanii wa Rap Harmorapa aliyepata umaarufu mkubwa baada ya kufananishwa na msanii kutoka kundi la WCB Hamonize amesema hana mpango wa kubadilisha jina lake “labda iongezeke a.k.a tu”.

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Hamorapa amesema maneno ya watu kuwa ameamua kujiweka upande wa Alikiba ingawa ameshindwa kujizuia kuonesha mahaba yake kwa msanii huyo.

“Mi sijali watu watakaosema mimi ni team Kiba kwa kuwa niliamua kumpigia Alikiba magoti ile ilitokana na heshima na amefanya vitu vikubwa na kuwakilisha nchi yetu vizuri, kwa mimi namuhusudu saana Ali Kiba”. Alisema Hamorapa”.

Hata hivyo Hamorapa amewapa ujumbe watu ambao wamamsema vibaya kwamba hawezi kuimba, wanapaswa kutambua kwamba wanavyomsema vibaya wanamfanya aongeze juhudi na kujua vingi kila siku kwa kutumia zile ‘diss’ wanazompa.

Mtazame hapa:-

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364