-->

Aunt Ezekiel: Huu Ndio Wakati Wangu wa Kupata Watoto Zaidi

MSANII wa filamu za Bongo, Aunt Ezekiel, amedai kwamba anatamani kupata watoto zaidi kwa kuwa huu ndio wakati wake wa kufanya hivyo na hajui atapata watoto wangapi katika maisha yake.

Aunt Ezekiel ambaye yupo kwenye uhusiano na dansa wa msanii Diamond Platnumz, Mose Iyobo, amesema kwa kuwa ndio wakati wake wa kufanya maamuzi sahihi na haoni idadi kamili ya watoto atakaokuwa nao katika familia yake na Iyobo.

“Nilitamani kuitwa mama sasa naitwa mama, naomba Mungu anisaidie nikuze familia yangu na anibariki nipate watoto wengine kwa kuwa watoto ndiyo furaha yangu zaidi,” alisema Aunt Ezekiel mwenye mtoto anayeitwa Cookie.

“Mtoto wangu wa pili natamani awe wa kiume na wengine zaidi ambao hata sijui watakua wangapi watakaokuwa na jinsia yoyote nitafurahi kwa kuwa tamaa yangu ni kuwa na watoto wengi,” alisisitiza.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364