-->

VIDEO: Sirro Akoleza Moto Wakazi wa Mabondeni

Dar es Salaam: Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema watu wote wanaoishi mabondeni watoke mara moja kwa sababu kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha na ambaye hatafanya hivyo atakamatwa.

amishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Jumanne), Sirro amesema tayari amewaagiza Ma OCD na wakuu wa upelelezi kuanza oparesheni hiyo mara moja na kuhakikisha hasalii mtu katika mabonde.

Sirro amesema watakaokamatwa watapelekwa polisi kwa ajili ya mahojiano kisha kupelekwa mahali ambapo wataona inafaa.

“Kuendelea kukaa mabondeni kuhatarisha maisha yako. Sisi tunadhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao hivyo hatuwezi kuruhusu kuona watu wanaendelea kufa. Tukikukuta katika mabonde yaliyokubuhu takukamata na familia yako, lazima tutumie shuruti maana binadamu wengine bila kushurutishwa hawaendi,”amesema Sirro.

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364